Wednesday, June 12, 2013

MCHEZAJI CHIPUKIZI WA CONGO BRAZZAVILLE AFARIKI KWA MALARIA.

MCHEZAJI chipukizi mwenye umri wa miaka 18 wa kimataifa wa Congo Brazzaville ameripotiwa kufariki jana baada ya kuugua malaria katika mji mkuu wan chi hiyo Brazzaville. Stevy Epako alikuwa ni mshambuliaji wa klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Jamhuri ya Kidempkrasia ya Congo-DRC ya Don Bosco ambayo inamilikiwa na mtoto wa kiume wa rais wa klabu ya TP Mazembe Moise Katumbi Chapwe. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, mchezaji huyo alikuwa akisumbulia na homa kali pamoja na malaria na alikimbizwa katika hospitali moja jijini Lubumbashi kwa ajili ya matibabu. Epako alikuwa nahodha wa kikosi cha timu ya taifa kwa vijana chini ya umri wa miaka 18 ya Congo Brazzaville na alikuwa akihesabika kama mmoja ya wachezaji wenye vipaji anayechipukia nchini humo.

No comments:

Post a Comment