Wednesday, June 12, 2013
WACHEZAJI WAWILI TOGO WAGOMA KWENDA LIBYA KWASABABU ZA KIUSALAMA.
WACHEZAJI wawili wa timu ya taifa ya Togo wameweka wazi kuwa hawatarajii kusafiri na kikosi hicho kwenda Libya mwishoni mwa wiki ijayo kwa ajili ya mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kutokana na sababu za kiusalama. Kiungo wa Marseille ambaye ia ndio nahodha wa Togo, Alaixys Romao na mshambuliaji Jonathan Ayite ambaye anacheza klabu ya Brest amejitoa katika kikosi cha nchi hiyo kinachonolewa na Didier Six ambacho kitacheza mechi yake Ijumaa jijini Tripoli. Romao alidai mapema kuwa anafikiri kama wanatupiwa katika mdomo wa simba kwa kuwapeleka katika mji wa Benina ulio karibu na Benghazi ambapo watu zaidi ya 30 wameuwawa katika matukio tofauti. Hata hivyo Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jumatatu lilihamisha mchezo huo kwenda kuchezewa katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli. Kama wachezaji hao wakishikilia msimamo huo kikosi cha Togo kitapata pigo kubwa kwa mechi yao ijayo baada ya nyota wengine kama Emmanuel Adebayor na golikipa mkongwe Kossi Agassa kukosekana katika mechi mbili zilizopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment