TIMU ya mpira wa kikapu Miami Heat imefanikiwa kutwaa taji la pili mfululizo la Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani-NBA baada ya kuifunga timu ya San Antonio Spurs kwa vikapu 95-88 katika fainali ya saba iliyofanyika katika Uwanja wa American Airlines uliopo jijini Miami, Florida. San Antonio walibakiza kidogo kulinyakuwa taji hilo Jumanne kabla ya Miami kupambana na kushinda hivyo kuzifanya timu hizo kutoka sare ya kufunga 3-3 katika fainali ya sita kati ya saba ambazo wanatakiwa kucheza.
Katika mchezo wa Alfajiri kuamkia leo nyota wa timu ya Heat, LeBron James mwenye umri wa miaka 28 alifanikiwa kuisadia vyema timu yake kwa kufunga vikapu 37 na kutajwa kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi katika ligi hiyo kwa mara ya pili mfululizo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo James ambaye aliingia matatani baada ya kudaiwa kucheza chini ya kiwango katika mechi muhimu amesema anajisikia fahari kunyakuwa taji hilo katika uwanja wao wa nyumbani na yote yaliyopita yanabaki kuwa historia.
No comments:
Post a Comment