Monday, June 3, 2013

MOURINHO ATUA RASMI CHELSEA KWA MKATABA WA MIAKA MINNE.

KLABU ya Chelsea imemteua tena Jose Mourinho kuwa meneja wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne. Mourinho ambaye ni raia wa Ureno atachukua nafasi ya Rafael banitez aliyejiunga na Napoli baada ya kuinoa klabu hiyo kwa miezi sita. Hii ni mara ya pili kwa Mourinho kurejea Stamford Brigde kama kocha kocha baada ya kuondoka miaka sita iliyopita. Mourinho ndiye alikuwa chaguo la kwanza la mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich baada ya kuinunua klabu hiyo mwaka 2003 na ndiye kocha pekee kati ya tisa waliopita klabuni hapo kuanzia kipindi hicho aliyeipa mafanikio zaidi.

No comments:

Post a Comment