Tuesday, June 4, 2013

NATAKA KUMSAIDIA MESSI AENDELEE KUNG'ARA ZAIDI ULAYA - NEYMAR.

MSHAMBULIAJI nyota mpya wa klabu ya Barcelona, Neymar amesema anataka kumsadia nyota wa klabu hiyo Lionel Messi aendelee kung’ara duniani baada ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho wake kutoka klabu ya Santos. Neymar mwenye umri wa miaka alikamilisha uhamisho wake wenye thamani ya euro million 57 na kumaliza utata wa miezi kadhaa juu ya mstakabali wa nyota huyo. Akihojiwa mara baada ya kutambulishwa rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki katika uwanja wa Camp Nou, Neymar amesema anataka kuisaidia timu kwasababu Barcelona ni zaidi ya klabu na pia anataka kumsadia Messi aendelee kung’ara zaidi. Nyota huyo aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ndoto zake kucheza katika klabu ambayo inahesabika kama mojawapo ya klabu bora duniani huku akizungukwa na wachezaji nyota. Neymar anaondoka Santos akiwa ameshinda Kombe la Brazil mwaka 2010, Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini mwaka 2011 huku akiwa amefunga mabao 138 katika mechi 229 alizocheza akiwa katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment