JOSE Mourinho anategemea kuchaguliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea mwishoni mwa wiki hii baada ya kuondoka rasmi katika klabu ya Real Madrid ya Hispania. Mourinho ambaye ni raia wa Ureno amemaliza amekuwa na msimu mbaya na Madrid baada ya kushindwa kuelewana na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na viongozi wa benchi lake la ufundi huku akishindwa kutwaa taji lolote msimu huu. Mourinho aliwahi kuzungumzia nia yake ya kwenda mahali ambapo anapendwa baada ya Madrid kuenguliwa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Borussia Dortmund. Akihojiwa mara ya kumalizika kwa mechi yake ya mwisho akiwa Madrid, Mourinho amesema anategemea kwenda jijini London kufanya mazungumzo na ni mategemeo yake atatajwa kama meneja mpya wa klabu hiyo mwishoni mwa wiki. Mara ya kwanza Mourinho kuinoa Chelsea ilikuwa ni mwaka 2004 baada ya kuingoza Porto kushinda taji la Ligi ya Mabingwa, na kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu, moja ya FA na mawili ya Kombe la Ligi kabla ya kuondoka mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment