Monday, June 3, 2013

ALLEGRI KUBAKIA SAN SIRO.

MENEJA wa klabu ya AC Milan ya Italia, Massimiliano Allegri ataendelea kubakia San Siro baada ya kufanya mazungumzo na rais wa klabu hiyo Silvio Berlusconi na Mtendaji Mkuu Adriano Galliani. Mustakabali wa Allegri katika klabu hiyo ulikuwa mashakani katika wiki za karibuni baada ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 kuisaidia timu hiyo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa katika mechi ya mwisho huku mahasimu wao AS Roma wakiripotiwa kutaka kumchukua kocha huyo. Hata hivyo hatimaye Allegri na viongozi wa klabu hiyo walikaa chini na kufanya mazungumzo baada ya mara kadhaa kikao chao kuahirishwa kutokana na sababu mbalimbali. Allegri alichukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo mwaka 2010 na kuiongoza kushinda taji la Ligi Kuu nchini Italia katika msimu wake wa kwanza.

No comments:

Post a Comment