Tuesday, June 11, 2013
NITATESA KATIKA VIWANJA VYA NYASI - FEDERER.
MCHEZAJI tenisi nyota anayeshika namba mbili katika orodha za ubora duniani, Roder Federer amesema ana uhakika kufanya vyema katika michuano ya viwanja vya nyasi baada ya kutoka kapa katika viwanja vya vumbi. Federer ambaye ni raia wa Switzerland alienguliwa na Jo-Wilfred Tsonga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa iliyomalizika Jumapili iliyopita kwa Rafael Nadal kutawadhwa bingwa mpya wa michuano hiyo kwa mara ya nane. Pamoja na kutofanya vyema katika michuano hiyo Federer amesema ana uhakika wa kfanya vyema katika michuano ya Wimbledon itakayofanyika jijini London wiki mbili zijazo baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu zaidi. Nyota huyo ambaye anakwenda kwenye michuano hiyo kama bingwa mtetezi tayari ana mataji 17 ya Grand Slam katika kabati lake lakini bado anaonekana ana uchu wa kuongeza mataji mengine zaidi mwakubwa kwa mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment