Tuesday, June 11, 2013
MERCEDES, PIRELLI KUFIKISHWA KIZIMBANI KWA KUJARIBU MAGURUDUMU ISIVYOPASWA.
TIMU ya Marcedes na kampuni na magurudumu ya Pirelli wanatarajiwa kuitwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Langalanga kujibu tuhuma za kujaribu magurudumu kinyume cha cha utaratibu. Hatua hiyo imekuja kufuatia Pirelli kutumia Mercedes kwa ajili ya majaribio ya magurudumu yake kwa muda siku tatu Mei mwaka huu. Shirikisho la Kimataifa la mashindano ya Langalanga-FIA limedai kuwa hatua hiyo ya Pirelli inaweza kuwa inekiuka sheria za mashindano hayo ambayo huzuia majaribio katika kipindi cha katikati ya msimu wa masgindano hayo. Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa Juni 20 mbele ya jopo la majaji jijini Paris huku FIA wakidai kuwa uamuzi utakaofikiwa na mahakamani utatangazwa haraka iwezekanavyo. Hatua ya usikilizwaji wa kesi hiyo imekuja baada ya mahasimu wa Marcedes timu ya Red Bull na Ferrari kulalamika kuwa Marcedes walitumia gari lao jipya lililotoka mwaka huu kwa ajili ya majaribio hayo ya kilimeta 1,000 jijini Barcelona.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment