Tuesday, June 11, 2013

MAN UNITED YAONYESHWA TAA YA KIJANI KWA FABREGAS NA LEWANDOWSKI.

KLABU ya Manchester United imezidi kujiamini kwamba inaweza kuwasajili Cesc Fabregas na Robert Lewandowski katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi baada ya wachezaji hao wawili binafsi kuwatia moyo. Meneja mpya wa United David Moyes angependa kuwaleta wachezaji hao klabuni hapo kabla ya hawajasafiri kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya huko Asia na Australia mwezi ujao. Inaeleweka kuwa Fabregas ambaye anacheza Barcelona baada ya kuondoka Arsenal miaka miwili iliyopita na Lewandowski ambaye ni mshambuliaji Borussia Dortmund wote wameonyesha nia ya kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu na United wanaamini wanaweza kufanikiwa katika hilo. Fabregas mwenye umri wa miaka 26 amekuwa mtu asiye na furaha sana toka atue Barcelona baada ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza huku Lewandowski akihamishia mapenzi yake Uingereza baada ya dili lake kwenda Bayern Munich kushindikana. Kama nyota huyo wa Dortmund akitua Old Traford itaongeza msukumo wa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Wayne Rooney ambaye aliomba kuondoka katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment