Friday, June 14, 2013

BOLT ATAMBA MBIO ZA MITA 200 ZA OSLO.


BAADA ya kuchemsha katika mbio za mbio za mita 100 zilizofanyika jijini Rome wiki moja iliyopita bingwa mara sita wa medali za dhahabu za olimpiki, Usain Bolt amefanikiwa kurejesha heshima yake kwa kushinda mbio za mita 200 za Diamond League zilizofanyika jijini Oslo. Mara ya kwanza mbio hizo zilivurugika baada ya Churundy Martina kuanza kukimbia kabla ya wenzake hivyo kuenguliwa na mbio hizo kuanza tena ambapo Bolt alishinda kirahisi akiwaacha wenzake mbali kwa kutumia muda wa sekunde 19.79. 
Bolt amekuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia chini ya sekunde 20 katika mbo za mita 200 msimu huu aliwasili jiji Oslo baada kushindwa na Justin Gatlin katika mbio za mita 100 zilizofanyika jijini Rome wiki iliyopita. Baadae Bolt aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa ingawa kulikuwa na baridi sana lakini alijitahidi kukimbia kwa kasi kadri alivyoweza na kama alivyoahidi hivyo anashukuru kwa kufanya vyema. Mshndi wa pili katika mbio hizo alikuwa ni Jasyma Saidy Ndure wa Norway huku mshindi wa tatu akiwa James Ellington wa Uingereza.


No comments:

Post a Comment