Friday, June 14, 2013

PRINCE-BOATENG AREJEA GHANA.

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Ghana, GFA, Kwesi Nyantakyi amethibitisha kuwa Kevin-Prince Boateng ameomba kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo. Katika mahojiano maalumu na kipindi cha Soccer Afrika kinachorushwa na luninga ya Super Sport ya Afrika Kusini jana usiku, Nyantakyi alithibitisha taarifa hizo baada ya uvumi uliozagaa nchini Ghana juu ya kurejea kwa nyota huyo siku tatu zilizopita. Rais huyo amesema kabla kocha wa timu hiyo Kwesi Appiah hajachagua kikosi kwa ajili ya mechi dhidi ya Sudan Boateng tayari aliwasiliana na kocha kuwa yuko tayari kuitwa lakini bahati mbaya wiki moja kabla ya mchezo huo akaumia wakati wakiwa mazoezini na klabu yake ya AC Milan. Boateng ambaye amewahi kucheza katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 19 cha timu ya taifa ya Ujerumani kabla ya kubadilisha uraia mwaka 2010, hajaichezea Ghana kwa miezi 18 kutokana na majeraha hivyo kuamua kujitoa kwenye timu hiyo kwa muda.

No comments:

Post a Comment