Friday, June 14, 2013

VILABU VINGI VINANIHITAJI.

BEKI wa zamani wa klabu ya Barcelona, Eric Abidal amesema kuna vilabu vingi ambavyo vinahitaji saini yake katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Abidal mwenye umri wa miaka 33 kwasasa ni mchezaji huru baada ya Barcelona kuamua kutomuongeza mkataba mwingine. Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi amesema kwasasa yupo likizo nab ado hajapokea ofa yoyote rasmi lakini tayari ana mawasiliano na vilabu kadhaa ingawa hakuna chochote walichozungumza. Abidal amesema anataka kupata muda zaidi ili kufikiria klabu ya kwenda kwasababu sasa hivi sio kijana tena kwani ana mke na watoto hivyo lazima awashirikishe kuhusiana na uamuzi wowote atakaochukua. Mapema mwezi huu Abidal alionyesha nia ya kumalizia soka lake katika klabu ya AS Monaco ambayo ndio alianzia akiwa na umri wa miaka 21.

No comments:

Post a Comment