KLABU ya Flamengo ya nchini Brazil imemteua Mano Menezes kuwa kocha mpya wa klabu hiyo ikiwa ni kazi yake ya kwanza toka atimuliwe kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo Novemba mwaka jana. Menezes mwenye umri wa miaka 51 atachukua nafasi ya Jorginho ambaye alieunguliwa baada ya kusimimia mechi 14 pekee na kuwa kocha wa tatu kutimuliwa katika klabu hiyo kwa mwaka huu. Kocha huyo aliinoa Brazil kwa kipindi cha miaka miwili lakini alitimuliwa baada ya viongozi wa soka baada ya kudai kuwa nchi hiyo imeachwa imesimama na Hispania na kama wanataka kuwakuta lazima wawe na mipango ya muda mrefu. Menezes alianza kuchomoza mwaka 2005 baada ya kuipandisha daraja timu ya Gremio kutoka daraja la pili kabla ya miaka miwili baadae kuifikisha klabu hiyo fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini. Baadae kocha huyo alijiunga na Corinthians na kuisadia kuitoa katika ligi daraja la pili na kuipandisha mpaka Ligi Kuu mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment