Tuesday, July 16, 2013

ADIDAS YASIMAMISHA MKATABA WAKE WA UDHAMINI NA GAY KWASABABU YA MADAWA.

KAMPUNI ya vifaa vya michezo ya Adidas imesimamisha mkataba wake wa udhamini na mwanariadha nyota wa mbio fupi Tyson Gay wa Marekani baada ya kukutwa na chembechembe za dawa za kuongeza nguvu. Msemaji wa kampuni alidai kuwa awameshtushwa na tuhuma hizo kwa Gay na hata kama bado hajakutwa na hatia ya kosa hilo moja kwa moja kampuni itasimamisha udhamini wake mpaka hapo hukumu itakapotolewa. Gay mwenye umri wa miaka 30, ndio mwanariadha wa pili mwenye kasi zaidi duniani katika mbio za mita 100 akiwa sambamba na Yohan Blake wa Jamaica na pia ndiye mwanariadha aliyeweka rekodi ya kasi zaidi kwa mwaka huu. Nyota huyo ambaye aliwahi kuwa bingwa wa dunia katika mbio za mita 100, 200 na mita 400 kupokezana vijiti mwaka 2007 alishindwa kukata tuhuma hizo na kudai kuwa alimwamini mtu ambaye alimwangusha na hivyo atapokea adhabu yoyote atakayopewa.

No comments:

Post a Comment