Saturday, July 6, 2013

AM NOT INVISIBLE - BOLT.

MWANARIADHA nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica Usain Bolt amedai kuwa yeye ni mwanariadha kama walivyo wengine hivyo sio ajabu kushindwa. Kauli hiyo ya Bolt imekuja wakati akijiandaa na mashindano ya Diamond League yatakayofanyika jijini Paris baadae leo ambapo atakimbia mbio za mita 200. Bolt ambaye ni bingwa mara sita wa michuano ya olimpiki atachuana na mjamaica mwenzake warren Weir na nyota mwingine mwenye kasi zaidi kwa mwaka huu Tyson Gay wa Marekani. Bolt amesema kama akifanikiwa kushinda mbio hizo za Paris anatakuwa amejiweka fiti kwa ajili ya kuchuana kwenye mashindano ya Riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi mwezi ujao.


No comments:

Post a Comment