Saturday, July 6, 2013

GAZZA AWEKWA LUPANGO KWA ULEVI.

MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Paul Gascoigne maarufu kama Gazza amekamatwa baada ya kufanya fujo wakati amelewa katika kituo cha treni. Gazza mwenye umri wa miaka 46 ambaye ametoka kupatiwa matibabu ya kunywa pombe kupindukia nchini Marekani mapema mwaka huu alishikiliwa na polisi baada ya kufanya tukio hilo huko Hertfordshire. Msemaji wa Polisi wa eneo hilo alithibitisha kuwa wamemkamata nyota huyo wa zamani baada ya kupigiwa simu na mlinzi wa eneo la kituo cha treni kwamba anafanya fujo kutokana na kulewa pombe kupitiliza. Msemaji huyo aliendelea kudai kuwa walimshikilia Gazza kwa saa 12 na baadae kuwekewa dhamana na uchunguzi wa polisi unaendelea kuhusiana na tukio hilo kabla ya kupelekwa mahakamani. Mapema mwaka huu baadjhi ya wachezaji walijichangisha na kupata fedha ambazo zilimsadia Gazza kumpeleka Marekani kwa ajili ya matibabu ya kuzuia ulevi uliopindukia baada ya hali yake kuwa mbaya.

No comments:

Post a Comment