Saturday, July 6, 2013

WACHEZAJI WAWILI WA SERIE A WAFUNGIWA NA FIFA KWA KUPANGA MATOKEO.

WACHEZAJI wawili wa vilabu vya Ligi Kuu nchini Italia marufu kama Serie A wamefungiwa miezi mitatu na siku 10 na kutozwa faini ya euro 10,000 kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kutengeneza mikakati ya kupanga matokeo ya mechi zao. Wachezaji ambao ni mshambuliaji wa klabu ya Torino, Paulo Vitor de Souza Barreto na beki wa klabu ya Genoa Giovanni Marchese walitandikwa adhabu hiyo na Shirikisho la Soka nchini Italia baada ya kushindwa kujitetea kutokana na tuhuma hizo. Mbali na hao IFF pia ilimfungia Davide Lanzafame ambaye anacheza kwa mkopo katika ya Honved ya Hungary akitokea klabu ya Catania, miezi 16 na faini ya euro 40,000 baada ya yeye pia kukutwa na hatia katika makosa ya kupanga matokeo wakati akiwa Italia. Hukumu hiyo imetolewa bada ya kufanyika uchunguzi katika mechi zilizohusisha timu ya Bari katika msimu wa 2008-2009 wakati ikiwa daraja la pili na msimu wa 2010-2011 wakati ikiwa ligi kuu.

No comments:

Post a Comment