Saturday, July 6, 2013

BLATTER KUFANYA ZIARA MASHARIKI YA KATI.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter anatarajiwa kufanya ziara Mashariki ya Kati ili kujaribu kuondoa vikwazo vya Israel kuwazuia wanasoka wa Palestina kusafiri kuingia nchi humo. Katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa FIFA Blatter amesema katika ziara yake hiyo anatarajia kukutana na rais wa Palestina Mahmoud Abbas na baada kuzungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Blatter amesema mbali na kukutana na viongozi hao wa juu pia atazungumza na viongozi wa mashirikisho ya soka wa mataifa hayo mawili pamoja na kuangalia miradi ya maendeleo ya soka huko na pia kutembelea kambi ya wakimbizi wa Syria iliyoko huko Jordan. Palestina wamekuwa wakichukizwa na majeshi ya usalama ya Israel ambayo ndio wanamiliki maeneo ya Gaza kuwazuia wanamichezo kusafiri kwa uhuru katika maeneo hayo kwa sababu za kiusalama.

No comments:

Post a Comment