Wednesday, July 3, 2013

BARCELONA ILIFANYA SAHIHI KUMSAJILI NEYMAR - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi anaamini kuwa klabu hiyo ilifanya jambo sahihi kumsajili Neymar katika kampeni yao ya kutetea taji La Liga na kufanya vyema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Neymar mwenye umri wa miaka 21 alikamilisha usajili wake uliogharimu kiasi cha euro milioni 57 akitokea Santos Juni mwaka huu ingawa hatahivyo wakosoaji wanadai Barcelona ilifanya makosa kutumia fedha nyingi kumsajili nyota huyo ambaye hajawahi kucheza Ulaya. Lakini baada ya kufunga mabao manne katika michuano ya Kombe la Shirikisho ilikiwemo bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa Dunia Hispania wakooaji hao watakuwa wameshapata majibu ya maswali yao na Messi anategemea nyota huyo kufanya makubwa zaidi atakapokuwa Barcelona. Messi amesema anategemea Neymar ataleta mchango mkubwa katika klabu hiyo kama akiendelea kucheza katika kiwango cha juu kama ilivyo kwa timu yake ya taifa na Santos. Barcelona ilifanikiwa kunyakuwa taji la La Liga msimu uliopita lakini walipata kipigo kikubwa kutoka Bayern Munich kwenye mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo waling’olewa kwa kufungw ajumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili walizocheza.

No comments:

Post a Comment