Wednesday, July 3, 2013

UBAHILI WAENDELEA KUITESA ARSENAL KWENYE USAJILI WA HIGUAIN.

MARA baada ya kuinasa saini ya nyota wa klabu ya AJ Auxerre, Yaya Sanogo klabu ya Arsenal sasa inapambana kumsajili nyota wa klabu ya Real Madrid, Gonzalo Higuain. Klabu hizo mbili zimekuwa katika mvutano kuhusu ada ya uhamisho wa nyota huyo ambapo Arsenal wameonekana kuwa tayari kutoa kitita cha euro milioni 25, wakati Madrid wao wanataka ada iwe euro milioni 25.5. Kumekuwa na taarifa kuwa Arsenal wameshafikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo ambapo ataanza na mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki, mshahara ambao utamfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi kwenye klabu hiyo wakiwemo Theo Walcott na Thomas Vermaelen. Higuain ambaye nia raia wa Argentina inasenekana alikuwa akilipwa kiasi cha paundi 64,000 kwa wiki akiwa Madrid.

No comments:

Post a Comment