KLABU ya Barcelona italazimika kuilipa klabu ya Santos nyongeza ya euro milioni mbili kama mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Neymar atachaguliwa katika nafasi tatu za juu katika orodha ya tuzo ya Ballon d’Or kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Barcelona walifanikiwa kupata saini ya nyota huyo wa kimataifa wa Brazil kwa uhamisho wenye thamani ya euro milioni 57 lakini Santos wataambulia kiasi cha euro milioni 9.35 katika ada hiyo. Kiasi cha euro milioni 40 kililipwa kwa watu wengine akiwemo baba yake Neymar wakati euro milioni 7.65 zilizobakia ziligawanywa katika kampuni mbili zilizokuwa zikimiliki sehemu ya usajili wake ambazo ni Teisa Group na DIS. Santos inaweza kupata euro milioni mbili zaidi kama Neymar mwenye umri wa miaka 21 akifanikiwa kufanya vyema akiwa Barcelona na kushika nafasi tatu za juu kwenye tuzo hizo ambazo huandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.
No comments:
Post a Comment