Thursday, July 11, 2013

USAJILI WA ROBINHO KWENDA SANTOS WAKWAMA.

KLABU za AC Milan ya Italia na Santos ya Brazil zimethibitisha kuwa mpango wa mshambuliaji nyota wa Milan, Robinho kwenda Santos katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi umekwama. Klabu hizo mbili zilishindwa kufikia makubaliano ya ada ya uhamisho kwa mchezaji huyo, huku Neymar mwenyewe naye akishindwa kuafikiana na Santos kuhusu mshahara wake na mambo mengine binafsi. Ofisa Mkuu wa Milan, Adriano Galliani alithibitisha kwamba mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yalishindikana na kuwa nyota huyo wa zamani wa Real Madrid ataendelea kubakia Rossoneri. Robinho ana mkataba na Milan ambao unamalizika Juni mwakani.

No comments:

Post a Comment