Sunday, July 7, 2013

BARTOLI ATAWADHWA KUWA MALKIA MPYA WA WIMBLEDON.

MWANADADA nyota katika tenisi, Marion Bartoli amefanikiwa kushinda taji lake la kwanza la michuano ya Grand Slam baada ya kumgaragaza Sabine Lisicki wa Ujerumani kwa 6-1 6-4 kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Wimbledon. Bartoli ambaye anashika namba 15 katika orodha za ubora kwa upande wanawake alitumia dakika 30 pekee kushinda seti ya kwanza wakati mpinzani wake Lisicki akionekana kushindwa kumudu vishindo katika fainali yake ya kwanza ya Grand Slam. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Bartoli amesema haamini kama amenyakuwa taji hilo na alikuwa akijisikia kucheza kwa kiwango chake cha juu huku kila kitu alichofanya kikimuendea sawa. Michuano hiyo inaendelea tena baadae kwa mchezo wa fainali kwa upande wa wanaume ambapo Andy Murray wa Uingereza anayeshika namba mbili katika orodha za ubora atachuana na Novak Djokovic wa Serbia anayeshika namba moja katika orodha za ubora.

No comments:

Post a Comment