WAZIRI Mkuu David Cameron na Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza wamekuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliotoa pongezi kwa mchezaji tenisi nyota wan chi hiyo Andy Murray kwa kunyakuwa taji la michuano ya Wimbledon. Wachezaji nyota na watu wengine maarufu nchini humo pia walitoa pongezi zao kwa Murray mwenye umri wa miaka 26 baada ya kuwa Muingereza wa kwanza kunyakuw ataji la michuano hiyo toka Fred Perry alipofanya hivyo mwaka 1936, kwa kumfunga Novak Djokovic kwa seti 3-0.
Cameron ambaye alikuwepo uwanjani kushuhudia mtanange huo alimpongeza Murray kwa kuonyesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo na kuweka historia mpya katika mchezo huo nchini Uingereza. Mwandishi wa BBC katika kasri ya kifalme nchini humo, Peter Hunt alibainisha kuwa Malkia alimtumia ujumbe binafsi Murray kumpongeza kwa kufanikiwa kushinda taji hilo.
No comments:
Post a Comment