Wednesday, July 17, 2013

BLAKE AJITOA MASHINDANO YA RIADHA YA DUNIA.

BINGWA mtetezi wa michuano ya riadha ya dunia ya mbio fupi za mita 100, Yohan Blake amejiengua katika mashindano ya dunia yam bio hizo yanayotarajiwa kuwafanyika jijini Moscow kutokana na majeraha ya msuli. Blake raia wa Jamaica mwenye umri wa miaka 23 alijitoa katika michuano ya taifa ya nchi yake mwezi uliopita kutokana na majeraha hayo aliyopata Aprili mwaka huu. Blake alishinda mbi za michuano hiyo iliyofanyika jijini Daegu mwaka 2011 wakati Mjamaica mwenzake Usain Bolt alipoenguliwa kwa kosa la kudanganya. Wanairiadha wengine ambao hawatakuwemo katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao ni pamoja na Asafa Powell na Tyson Gay wa Marekani ambao wamejitoa baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

No comments:

Post a Comment