Monday, July 15, 2013

CAVANI ATUA PARIS KUKAMILISHA DILI LAKE LA KUHAMIA PSG.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Napoli ya Itali, Edinson Cavani ametua jijini Paris kumaliza taratibu za uhamisho wake kwenda klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, huku vyanzo vya karibu vikidai kuwa usajili wake wa euro milioni 64 utavunja rekodi nchini Ufaransa. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikuwa mfungaji bora Serie A msimu uliopita akifunga mabao 29 ametua jijini Paris mapema leo ni kuelekea katika moja ya hoteli zilizopo katikati ya jiji. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Cavani anatarajiwa kuchukuliwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo. Kama Cavani akifanikiwa kusaini mkataba huo na mabingwa hao wa soka nchini Ufaransa, ataungana na mchezaji mwenzake wa Napoli Ezequiel Lavezzi ambaye ni raia wa Argentina.

No comments:

Post a Comment