Tuesday, July 16, 2013

FIFA YAZIDI KUIKOMALIA CAMEROON.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limedai kuwa klabu ya Coton Sport ya Cameroon haitaruhusiwa kucheza mechi yao ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika mwishoni mwa wiki hii kwasababu ya adhabu iliyopewa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot na FIFA. Hatua ya kuzuiwa kwa klabu hiyo kunazidi kuleta utata katika michuano hiyo mikubwa kabisa ya vilabu barani Afrika huku mahasimu wa soka nchini Misri klabu ya Zamalek na Al Ahly ambao ndio mabingwa watetezi nao wakiwa hawajui hatma ya mechi baina yao kwasababu ya vrugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo. Timu nane zilizofanikiwa kuvuka hatua ya makundi, ndio zinatarajiwa kuchuana kutafuta washindi watakaocheza nusu fainali ya michuano hiyo katika mechi zao za kwanza mwishoni mwa wiki hii. FIFA imesema kuwa tayari wameshaanza mazungumzo kujaribu kutatua mgogoro wa Cameroon lakini mpaka sasa hakuna lolote lililofikiwa mpaka kuwashawishi kuondoa adhabu ya kuifungia nchi hiyo kushiriki michuano yoyote ya kimataifa waliyoitoa Julai 4 mwaka huu. Kufungiwa kwa Cameroon kumekuja kufuatia uchaguzi wa Juni 19 ambao Mohammed Iya alichaguliwa tena kuongoza Fecafoot pamoja na kukamatwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha wakati akiongoza kampuni ya Cotton Development Corporation inayomiliki timu ya Cotton Sport.



Kwa upnde mwingine Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF bado halijateua uwanja utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa Zamalek na Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Jumapili kutoka mamlaka za usalama kushindwa kuhakikisha ulinzi jijini Cairo pamoja na mji wa Alexandria kwasababu ya vurugu za kisiasa zinazoendelea.

No comments:

Post a Comment