Tuesday, July 16, 2013

FENERBAHCE, BESIKTAS ZAGONGA MWAMBA UEFA.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA, limesema kuwa klabu za Fenerbahce na Besiktas za Uturuki zimeshindwa rufani zao za kupinga adhabu ya kushiriki michuano inayoandaliwa na shirikisho hilo. Fernabahce ambao ilikuwa washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu walifungiwa kushiriki michuano yoyote ya Ulaya kwa misimu miwili huku Besiktas ambao walifuzu kushiriki michuano ya Europa League wao wamefungiwa msimu mmoja. Klabu zote mbili zinatuhumiwa na kashfa ya upangaji matokeo katika baadhi ya mechi za Ligi ya Kuu ya Soka nchini Uturuki mwaka 2011. Baada ya kugonga mwamba UEFA, klabu hizo bado zina haki ya kukata rufani katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS.

No comments:

Post a Comment