Friday, July 12, 2013

DIS WATISHIA KWENDA MAHAKAMANI KUHUSIANA NA SUALA LA UHAMISHO WA NEYMAR.

KAMPUNI ya DIS inayomiliki maduka makubwa nchini Brazil na ambao wanamiliki asilimia 40 ya haki za usajili wa Neymar wametishia kwenda mahakamani kuhusiana na mgao wao kwa nyota huyo katika usajili wake kwenda Barcelona. Kampuni hiyo inayoendeshwa na Idi Sonda imedai kuwa na haki ya kupata fedha zaidi juu ya makubaliano ya ziada kati ya klabu ya Santos na Barcelona ambayo yako nje ya ada ya uhamisho wake ambayo ilifikia kiasi cha euro milioni 57. Mkurugenzi Mtendaji wa DIS, Roberto Moreno ameomba kupewa taarifa kamili ya hati ya uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona ili kupata ufafanuzi kuhusu malipo ya baadae watakayopewa Santos. Moreno amesema mpaka kipindi hicho hawajaonyeshwa hati yoyote, hivyo atafunga safari kwenda makao makuu ya Santos kufuatilia hati hiyo na baada ya hapo wataamua kama watahitaji kwenda mahamani. Hatua ya kampuni hiyo imekuja kufuatia taarifa zilitolewa na vyombo vya habari nchini humo kwamba Santos watapata nyongeza ya euro milioni mbili kama mchezaji huyo atakuwemo katika orodha ya wachezaji watatu kwenye tuzo ya Ballon d’Or kwenye kipindi cha miaka mitano ijayo.

No comments:

Post a Comment