Friday, July 5, 2013
FECAFOOT WALALAMIKIA KUFUNGIWA NA FIFA.
SHIRIKISHO la Soka la Cameroon-FECAFOOT limeponda uamuzi wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA baada ya kufungiwa kushiriki michuano yoyote ya kimataifa kutokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka. Msemaji wa FECAFOOT Junior Binyam amesema uamuzi wa FIFA ni mbaya na unaweza kuharibu vipaji vya wachezaji chipukizi wakiwemo wale bora ambao wanataka kwenda Ulaya kujaribu bahati zao kwa sababu watakosa hati za unamihisho wa kimataifa. Cameroon ilitakiwa kucheza na Gabon Jumamosi katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani-CHAN lakini mechi hiyo haitakuwemo kutokana adhabu waliyopewa. FIFA ilifikia uamuzi wa kuifungia Cameroon katika mashindano ya kimataifa kwasababu ya serikali kuingilia maamuzi ya FECAFOOT kuhusiana na uchaguzi wa shirikisho hilo. Kama adhabu hiyo ikiendelea mpaka Septemba mwaka huu Cameroon pia itashindwa kucheza mechi yake ya mwisho ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Libya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment