MFANYABIASHARA bilionea wa Uingereza, Mohamed Al Fayed amemaliza miaka 16 akiwa mmiliki wa klabu ya Fulham kwa kuiuza klabu hiyo kwa biliobea wa Marekani Shahid Khan ambaye anamiliki timu ya Jacksonville Jaguars inayoshiriki Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu wa Kimarekani-NFL. Khan mwenye umri wa miaka 62, mjasiriamali bilionea anayejihusisha na biashara ya vipuri vya magari anakuwa Mmarekani wa sita kumiliki klabu katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Wakati akiwa mmiliki, Al Fayed mwenye umri wa miaka 84 raia wa Misri aliichukua Fulham wakati ikiwa daraja la tatu na kuipandisha mpaka ligi kuu na baadae mpaka kufikia kushiriki michuano ya Ulaya. Al Fayed amesema imekuwa ni fahari kubwa na heshima kuwa mwenyekiti wa Fulham katika kipindi cha miaka 16 ya kukumbukwa. Khan mzaliwa wa Pakistan ambaye alihamia marekani akiwa na umri wa miaka 16, ameajiri maelfu ya watu kupitia biashara yake ya vipuri vya magari ndani na nje ya nchi ya Marekani. Hakuna taarifa rasmi ya kiasi alichotoa Khana kuinunua klabu hiyo, lakini vyombo vya habari vimeripoti kuwa biionea huyo ameinunua Fulham kwa kiasi cha kati ya paundi miioni 150 na 200.
No comments:
Post a Comment