Monday, July 8, 2013
HENRY ATAJWA KATIKA KIKOSI CHA NYOTA WA MLS.
MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Ufaransa, Thierry Henry ni miongoni mwa wachezaji nyota 10 watakaounda kikosi kutoka katika Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS ambacho kitapambana na AS Roma ya Italia Julai 31 huko jijini Kansas. Henry mwenye umri wa miaka 35 mshambuliaji wa klabu ya New York Red Bull ambaye aliisadia Ufaransa kushinda Kombe la Dunia mwaka 1998, amefunga mabao sita katika mechi 17 alizoichezea timu hiyo msimu huu. Kabla ya kwenda Marekani mwaka 2010 akitokea klabu ya Barcelona, henry amewahi kucheza katika vilabu vya Juventus na Arsenal. Golikipa wa FC Dallas ambaye ni raia wa Peru Raul Fernandez, kiungo wa timu ya taifa ya Canada Will Johnson na Beki wa Kansas City Aurelien Collin ambaye ni raia wa Ufaransa ni miongoni mwa wachezaji wasiokuwa raia wa Marekani walioteuliwa katika kikosi hicho cha nyota wa MLS.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment