Monday, July 8, 2013

BLATTER KUZUNGUMZA NA ISRAEL KUJARIBU KUONDOA VIZUIZI VYA WACHEZAJI KATIKA MJI WA GAZA.

RAIS wa Shirikisho la Soka Dunia-FIFA Sepp Blatter amemwambia kiongozi wa michezo nchini Palestina kwamba atazungumza na maofisa wa Israel ili kujaribu kuondoa vizuizi vya kusafiri walivyowekewa wachezaji wa taifa hilo. Blatter alitarajiwa kukutana na ofisa mkuu wa soka nchini Israel kabla ya kuzungumza na kiongozi wa kisiasa wan chi hiyo waziri mkuu Benjamin Netanyahu kuzungumzia suala hilo. Palestina wamekuwa wakichukizwa na vikosi vya usalama vya Israel ambavyo vinalinda mji wa Gaza kuwazuia wanamichezo wa taifa hilo kusafiri kwa uhuru katika pande hizo mbili. Blatter amesema atakwenda Israel sio kwenda kukitetea Chama cha Soka cha Palestina lakini pia kutetea misingi ya kanuni za FIFA ambayo ni kuunganisha watu na sio kuwagawa.

No comments:

Post a Comment