Monday, July 8, 2013
RONALDO ATAJWA KATIKA ORODHA YA WACHEZAJI WATAKAOGOMBEA TUZO YA UNYAYO WA DHAHABU.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa katika orodha ya wachezaji 10 watakaogombani tuzo ya Unyayo wa Dhahabu kwa mwaka 2013. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa ureno atakuwa mchezaji wa kwanza wan chi hiyo kushinda tuzo hiyo ambayo ilianza kutolewa mwaka 2003 mahsusi kwa wachezaji waliozidi umri wa miaka 28. Mchezaji mwenzake wa Madri Iker Casillas na kiungo mahiri wa Barcelona Andres Iniesta ni miongoni wa nyota wengine walioteuliwa kugombea tuzo hiyo. Wachezaji waliwahi kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa kuangalia uwezo wake wa kipindi chote alichocheza soka na kiwango chake cha sasa, ni pamoja na Roberto Carlos, Ronaldinho, Francesco Totti na mshindi wa mwaka uliopita Zlatan Ibrahimovic. Wachezaji wanaweza kushinda tuzo hiyo mara moja pekee, ambapo sherehe zake hufanyika jijini Monaco kila mwaka toka ilipoanzishwa. Mbali na hao wengine waliokuwemo katika orodha ya mwaka huu ni pamoja na Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala, Andrea Pirlo anayekipiga Juventus, Didier Drogba kutoka Galatasaray, Frank Lampard-Chelsea, Miroslav Klose-Lazio, David Trezeguet-River Plate and David Beckham-Paris Saint-Germain.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment