MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kurejea mazoezini Julai 15 baada ya kupumzika kwa wiki moja pekee katika likizo yake kutokana na majukumu mbalimbali ambayo yamekuwa yakimtinga. Masimu wa 2012-2013 kwa mchezaji huyo nyota ulimalizika Juni 15 baada ya Argentina kuigaragaza Guatemala kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki, hivyo kumanisha kwamba nyota huyo angekuwa na mwezi mzima wa kupumzika kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Hata hivyo Messi mwenye umri wa miaka 26 alitumia nafasi hiyo kucheza mechi mbalimbali za hisani kuzunguka dunia na kumaliza ziara yake hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita huko Chicago, Marekani. Jumla ya ziara zote hizo Messi amesafiri kilimita zaidi ya 90,000 toka msimu wa ligi ulipomalizika akitembelea nchi za Argentina, Ecuador, Guatemala, Italia, Senegal, Colombia, Peru na Marekani. Nyota huyo amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya msuli mwishoni mwa msimu uliopita na mapumziko mafupi aatakayopata yatawapa uhakika mdogo madaktari juu ya afya yake kabla ya kuanza msimu mpya wa 2013-2014.
No comments:
Post a Comment