Thursday, July 4, 2013
JUHINHO AKATISHA MKATABA NA NEW YORK RED BULLS.
KIUNGO mahiri wa klabu ya New York Red Bulls, Juninho Pernambocano amekatisha mkataba wake na klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miezi saba pekee. Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Brazil ambaye anajulikana zaidi kwa utaalamu wake wa kupiga mipira ya adhabu ndogo, amecheza mechi 13 katika kipindi kifupi ambacho ameitumikia klabu hiyo na sasa anarejea nchini kwao kuungana na familia yake. Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Marekani, Andy Roxburgh alithibitisha kuondoka kwa nyota huyo na kuelelezea masikitiko yake kwa sababu wamempoteza mchezaji muhimu na mwenye kipaji. Juninho ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006, aliwashukuru mashabiki wa klabu hiyo na wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompa katika muda aliokuwepo hapo. Klabu hiyo inashika nafasi ya pili baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi ya nchi hiyo kwa upande wa mashariki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment