Thursday, July 4, 2013

CAS YAIAMURU TOGO KUMLIPA KOCHA WAKE WA ZAMANI DOLA 400,000.

MAHAKAMA ya Usuluhishi ya Michezo-CAS imeliamuru Shirikisho la Soka nchini Togo kumlipa kocha wake wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo kiasi cha dola 400,000 kwa kukatisha mkataba wake. Kocha huyo aitwaye Jean Thissen raia wa Ubelgiji alikuwa akiinoa Togo kati ya mwaka 2008 na 2009 kabla ya kutimuliwa na maofisa wa soka wan chi hiyo ambao walidai kuwa kocha huyo alikuwa na matatizo ya kiafya na hawezi kufanya kazi akiwa katika hali hiyo. Thissen baadae alifikia uamuzi wa kupeleka vipimo vyake vya afya vilivyoonyesha kuwa ana afya ya njema ya kufanya kazi kama kocha na baadae kupelekea malalamiko yake CAS akidai fidia ya dola 800,000. Katika taarifa yake CAS imedai kutuma taarifa za maamuzi waliyofikia kwa mawakili wa pande zote mbili huku maofisa wa Togo wakidai kukutana baadae kujadili suala hilo na hatua ya kuchukua.

No comments:

Post a Comment