SHIRIKISHO la Soka nchini Ufaransa-FFF limemuongeza adhabu ya kumfungia Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Leonardo mpaka kufikia miezi 13 baada ya kushindwa rufani yake ya kupunguziwa adhabu hiyo. Katika taarifa yake FFF imedai kuwa Leanardo alikata rufani kupinga kufungiwa kujishughulisha na shughuli za michezo mpaka Juni 30 mwakani. Katika picha video zinamuonyesha Leonardo ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil akimpamia mwamuzi Alexandre Castro kwa bega lake la kushoto wakati wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya PSG kutoka sare ya bao 1-1 na Valenciennes Mei mwaka huu. PSG ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini humo nao pia walikatwa alama tatu baada ya rufani ya Leonardo kupigwa chini.
No comments:
Post a Comment