Friday, July 5, 2013
MADEREVA WA LANGALANGA WATISHIA KUGOMA.
MADEREVA wa mashindano ya magari yaendayo kasi ya langalanga wametishia kususia michuano ya Grand Prix ya ujerumani itakayofanyika Jumapili ijayo kama kutatokea matatizo ya kupasuka magurudumu kama ilivyotokea katika mashindano ya British Grand Prix wiki iliyopita. Chama cha Madereva wa Langalanga-GPDA kimedai kuwa wanachama wake wameonyesha wasiwasi kuhusiana na matukio yaliyopita na kama yakijirudia tena watalazimika kujitoa kwa ajili ya usalama wao. Katika michuano ya wiki iliyopita madereva sita walipasukiwa na magurudumu wakati wakiwa katika mwendo kasi wakiwemo Lewis Hamilton wa timu ya Marcedes, Felipe Massa na Frnando Alonso wa Ferrari, Jean-Eric Vergne wa Toro Rosso, Esteban Gutierrez wa Sauber na Sergio Perez wa MacLaren. Tayari kampuni inayosambaza magurudumu ya Pirelli imeshabadilisha aina ya magurudumu yatakayotumika katika mashindano ya Grand Prix ya Ujerumani ili kuepusha matatizo yaliyojitokeza wiki iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment