Wednesday, July 17, 2013

LIGI KUU YA SOKA NCHINI MISRI YASIMAMISHWA KWASABABU ZA KIUSALAMA.

LIGI Kuu ya Soka nchini Misri imesitishwa kwasababu za kiusalama kufuatia jeshi la nchi hiyo kumuondoa rais Mohamed Mursi madarakani mapma mwezi huu. Shirikisho la Soka la nchi hiyo lilitangaza rasmi kusitisha msimu wa ligi wa 2012-2013 huku kukiwa kumebaki mzunguko mmoja msimu kumalizika na timu nne kucheza hatua ya mtoano kwa ajili ya kumpata bingwa. Kwa zaidi ya wiki mbili toka jeshi limuondoe Mursi baada ya maandamano makubwa ya kumpinga, kumekuwa na vurugu huku watu zaidi ya saba wakiripotiwa kufa katika mapigano baina waislamu waliokuwa upande wa Mursi na wengine waliokuwa wakimpinga rais huyo. Hii ni mara ya pili katia kipindi cha miaka miwili ligi kusimamishwa katikati ya msimu baada ya mapema mwaka jana ligi hiyo kusitishwa tena kutokana na vurugu zilizotokea Port Said na kusababisha vifo vya mashabiki wapatao 74.

No comments:

Post a Comment