Friday, July 5, 2013

MIAKA 100 YA KOMBE LA DUNIA KUADHIMISHWA ARGENTINA NA URUGUAY.

RAIS wa Chama cha Soka nchini Argentina-AFA, Julio Grondona amedai kuwa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA linataka michuano ya Kombe la Dunia 2030 kuandaliwa kwa pamoja na Uruguay na Argentina. Mwaka 1930, Uruguay ambao walikuwa mabingwa wa olimpiki, waliifunga Argentina kwa mabao 4-2 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia iliyochezwa katika Uwanja wa Centenario jijini Montevideo na kuhudhuriwa na mashabiki wapatao 80,000. Grondona ambaye pia ni mjumbe katika kamati ya utendaji ya FIFA amedai kuwa FIFA ingependa kucherekea miaka 100 ya Kombe la Dunia nchini Argentina na Uruguay ikiwa kama sehemu ya kumbukumbu ya mahali ilipofanyika michuano hiyo kwa mara ya kwanza. Grodona amedai kuwa tayari makubaliano baina ya mashirikisho ya nchi hizo yameshafikiwa na sasa wanasubiri muda ili kutuma maombi ya kuandaa michuano ya kipindi hicho. Nchi za Japan na Korea Kusini ndio pekee zilizoweza kuandaa michuano hiyo kwa pamoja mwaka 2002 toka kuanzishwa kwake mwaka 1930.

No comments:

Post a Comment