
Friday, July 19, 2013
MRUSHA KISAHANI WA JAMAICA NAYE AKUMBWA NA KASHFA YA MADAWA YA KUSISIMUA MISULI.
TASNIA ya riadha bado inaendelea kukumbwa na misukosuko baada ya Traves Smikle wa Jamaica anayecheza mchezo wa kurusha kisahani naye kukutwa na chembechembe za dawa ambazo zimepigwa marufuku. Smikle ambaye alishiriki katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini London mwaka jana alikutwa na dawa hizo katika mwili wake katika vipimo alivyofanyiwa wakati mashindano ya majaribio ya Jamaica Juni mwaka huu. Wanariadha wengine wa Jamaica ambao mpaka sasa wamekumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Asafa Powell, Sherone Simpson, Veronica Campbell-Brown na mrusha kisahani mwingine Allison Randall. Katika taarifa yake Smikle mwenye umri wa miaka 21 amesema atawajibika kwa chochote ambacho kimekutwa katika mwili wake ingawa hata hivyo alidai kutojua au kutumiwa kwa ridhaa yake madawa hayo yaliyokatazwa michezoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment