
Friday, July 19, 2013
MOYES ASISITIZA TENA KUWA HANA MPANGO WA KUMUUZA ROONEY.
MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa Wayne Rooney hawezi kuuzwa baada ya Chelsea kudai kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza ndio chaguo lao katika kipindi hiki cha usajili majira ya kiangazi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Sydney, Australia katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya, Moyes amesema msimamo wa klabu kuhusiana na mustakabali wa nyota huyo bado haujabadilika. Akitupiwa swali lingine kuhusiana na suala ofa iliyotolewa na United kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas, Moyes amesema hajajua suala hilo linaendeleaje lakini anategemea katika siku mbili zijazo atafahamishwa na maofisa wa United maendeleo yake. Ofa ya kwanza ya meneja mpya wa Chelsea Jose Mourinho kutaka kumsajili nyota huyo tayari imekataliwa na United lakini klabu hiyo bado imeendelea kufuatilia nyendo za nyota huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment