Saturday, July 20, 2013

VILANOVA AJIUZULU KWASABABU YA MARADHI.

MENEJA wa klabu ya Barcelona, Tito Vilanova amejiuzulu wadhifa huo ili aweze kuendelea na matibabu yake saratani ya koo. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa saratani katika koo Nevemba mwaka 2011 kabla ya tatizo hilo kurejea tena na kufanyiwa upsuaji mwingine Desemba mwaka jana pamoja na kupatiwa na matibabu ya mionzi jijini New York kwa wiki 10. Rais wa Barcelona, Sandro Rosell aliwaambia waandishi wa habari kuwa kukosekana kwa kocha huyo ni pigo kubwa kwa klabu hiyo lakini wanatakiwa kuyashinda magumu hayo na kuangalia jinsi ya kujipanga kwa ajili ya msimu ujao. Rosell amesema kwasasa wanaingia katika mchakato wa kutafuta kocha mpya na wanatarajia wiki ijayo watakuwa wameshapata mbadala wa Vilanova. Vilanova alichukua nafasi ya Pep Guardiola Juni mwaka jana baada ya kufanya kazi kama kocha msaidizi wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment