Wednesday, July 3, 2013
PIRELLI YARUSHA LAWAMA KWA TIMU KUHUSIANA NA SUALA LA KUPASUKA KWA MAGURUDUMU.
KAMPUNI magurudumu ya Pirelli imezilaumu timu zinazoshiriki mshindano ya magari yanayokwenda kasi ya langalanga kutofuata taratibu kufuatia kupasuka kwa magurudumu kadhaa katika mashindano ya British Grand Prix. Kampuni hiyo ya Kiitaliano inatarajia kutoa aina mpya ya magurudumu kwa ajili ya mashindano ya German Grand Prix mwishoni mwa wiki hii ili kuepuka matukio yaliyotokea wiki iliyopita. Lakini Pirelli imetoa angalizo kwa shirikisho la mchezo huo-FIA kuingilia kati na kuhakikisha timu zote zinayatumia magurudumu hayo kama inavyopaswa. Katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imedai kuwa magurudumu yake yanayotengenezwa kwa ajili ya mashindano ya mwaka huu hayahatarishi usalama wa madereva kwa namna yoyote kama yakitumiwa ipasavyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment