Wednesday, July 3, 2013
PUYOL AKANUSHA TETESI ZA KUSTAAFU.
NAHODHA wa klabu ya Barcelona, Carles Puyol amekanusha madai kuwa anaweza kustaafu soka katika kpindi hiki cha majira ya kiangazi na kubainisha kuwa anategemea kuongeza mkataba wake. Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 35 amelazimika kufanyiwa upasuaji kwa mara nne wa goti lake la kulia mwishoni mwa msimu uliopita na kupelekea kuzuka tetesi kuwa nyota huyo anaweza kutundika daluga. Hata hivyo akihojiwa nyota huyo alikana uvumi huo na kudai kuwa bado anataka kumaliza mkataba wake na klabu hiyo na kama itawezekana ataongeza mwingine. Puyol amesema kwasasa anapona taratibu lakini anaendelea vyema na ni mategemeo yake atakuwa fiti katika siku ya kwanza ya mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi. Puyol ambaye mkataba wake unamalizika Juni 2016, ni matunda ya shule ya vijana ya klabu hiyo na ametumia muda wake wote wa kucheza soka akiwa hapohapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment