MAWAKILI wa mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Carlos Tevez wamefanikiwa kumuondolea adhabu ya kuitumikia jamii kwasababu ya kuhamia nchini Italia. Badala ya adhabu hiyo mahakama ya Macclesfield ilimtaka mchezaji huyo kulipa kiasi cha paundi 3,000 ili kufuta kesi hiyo. Mshambuliaji alikuwa bado hajamaliza muda wa masaa 250 aliyopewa kufanya kazi za kijamii baada ya kukutwa na hati ya kuendesha gari wakati akiwa hana leseni. Mapema mwezi uliopita Tevez alisajiliwa na klabu ya Juventus akitokea City.
No comments:
Post a Comment