MWANARIADHA wa mbio fupi Usain Bolt amefanikiwa kurejesha taji lake la dunia katika mbio za mita 100 baada ya kushinda medali ya dhahabu katika mbio hizo akitumia muda wa sekunde 9.77 jijini Moscow. Bolt mwenye umri wa miaka 26 ambaye miaka miwili iliyopita alienguliwa katika michuano hiyo iliyofanyika jijini Daegu kwa kudanganya alifanikiwa kushinda mbio hizo pamoja na mvua iliyokuwa ikinyesha. Mpinzani wa karibu wa Bolt katika mbio hizo Justin Gatlin wa Marekani alishika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa sekunde 9.85 wakati nafasi ya tatu ilishikiliwa na Nesta Carter wa Jamaica aliyetumia sekunde 9.95. Akihojiwa mara baada yam bio hizo Bolt amesema amefurahi kushinda lakini alikuwa akihitaji kufanya vizuri zaidi hapo.
No comments:
Post a Comment