DYKE AITAKA FIFA KUFIKIRIA KUHAMISHA KOMBE LA DUNIA 2022 MBALI NA QATAR.
MWENYEKITI mpya wa Chama cha Soka cha Uingereza, Greg Dyke amelitaka Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufikiria kuhamisha michuano ya Kombe la Dunia 2022 mbali na Qatar. Qatar ilifanikiwa kupata nafasi ya kuandaa michuano hiyo miaka mitatu iliyopita pamoja na timu ya wakaguzi ya FIFA kukiri kuwa itakuwa hatari kubwa kutokana na joto kali katika nchi hiyo ya jangwa ambalo hukadiriwa kufikia nyuzi joto 50 kipindi cha kiangazi. Mara kadhaa akiwa amekataa kuhusu utata huo wa Qatar, rais wa FIFA Sepp Blatter hivi karibuni ametaka kamati yake ya utendaji kukutana Octoba mwaka huu ili kujadili kama michuano hiyo ihamishiwe katika kipindi cha majira ya baridi. Akihojiwa kuhusiana na hilo, Dyke amesema kuwa FIFA ina mawili ya kuchagua ambayo ni kuhamisha michuano hiyo katika kipindi cha baridi au kutafuta sehemu nyingine lakini kucheza michuano hiyo katika kipindi cha kiangazi haitawezekana.
No comments:
Post a Comment